Monday, January 12, 2009

Yanga kidume

Timu ya Yanga ya Dar ndio club kilichotoa wachezaji wengi zaidi katika michuano ya CECAFA inayoendelea nchini UG. Yanga ina kikosi kamili na reserve katika timu hizi za taifa ikiwa na jumla ya wachezaji 14! Yanga ina wachezaji katika timu za Kili stars, Zanzibar heroes na Harambee stars. Wachezaji hao ni pamoja na Nsajigwa, Chuji, Bonny, Bakari, Tegete, Makasi, Maftah na Ngassa. Zanzibar Heroes in Abdi Kassim na Haroub Cannavaro wakati Shikokoti, Baraza, Owino na Njoroge wanaiwakilisha Kenya.

No comments: