Monday, January 12, 2009

Chelski hoiiiiii

Watoto wa Abramovic jana usiku walikiona cha moto baada ya kuchapwa 3 mtungi na mashetani wekundi wa Manchester.
Nemanja Vidic aliifungia Man U goli la kwanza kwa mpira wa kichwa dakika ya 45 ya kipindi cha kwanza kabla ya Rooney hajafunga la pili baada ya kross maridadi ya Patrice Evra katika dakika ya 63.
Berbatov alihakikisha ushindi unabaki Old Traford baada ya kufunga goli la tatu kutokana na mpira wa adhabu wa Ronaldo.
Chelsea ambao walionekana kupooza walishindwa kabisa kuisumbua ngome ya Man U.
Katika mechi nyingine ya mapema jana jioni, Wigan wakiwa home ground JJB Stadium, waliiliza Tottenham goli moja bila na kuiongezea matatizo mkiani mwa ligi. Goli la Wigan lilipatikana katika dakika za majeruhi kupitia kwa Maynor Figueroa.
Kwa msimamo wa ligi ya Uingereza kong'oli hapa: http://soccernet.espn.go.com/tables?league=eng.1&cc=4716

No comments: