Sunday, January 11, 2009

Premier League mbinde tupu

English premier league inaendelea leo kwa mechi kali kati ya mashetani wekundu, Man United wakiwakaribisha wahasimu wao toka London, vijana wa kitajiri, Chelsea katika uwanja wa Old Traford.
Mechi hiyo inayotarajia kupigwa saa moja kamili kwa saa zetu za Afrika Mashariki inategemewa kuwa kali sana.
Sir Alex anatarajia mechi itakuwa kali sana na katika mahojiano na wahandishi jana, alidai kuwa hatajali kuingia mwenyewe uwanjani kukipiga ili tu timu yake ipate ushindi.
Mdau ntakuwa nawaletea vidokezo muhimu na magoli kadri mechi itakavokuwa inaendelea hapa hapa.
Mdau Ayoub wa Mwanza najua tumbo joto leo maana ni shabiki mkuu wa Man YU!
Katika mechi za jana, Liverpool walivutwa shati na vijana wa mkiani Stoke city kwa kutoka suluhu, Arsenal wakiokolewa na 'super-sub' wao Niclas Bendtner katika dakika za lala salama baada ya kupoke pasi ya Van persie na kuwafunga Bolton 1-0. Newcastle walitoka draw ya 2-2, huku Everton wakiibuka na ushindi wa goli 2-0 dhidi ya Hull na Black Cats sunderland wakisubiri hadi dakika za majeruhi kusawazisha dhidi ya mahasimu wao Middlesbrough.
Matokeo kamili ni kama hivi:
Stock City 0:0 Liverpool
Arsenal (Niclas Bendtner dk. 84)1:0 Bolton
Aston Villa (Davies dk19, Carson dk41 o.g) 2:1 West Brom (Morrison dk. 49)
Everton (Fellaini dk. 47, Cahill dk. 58 2:0 Hull
Middlesbrough (Alves dk. 45 1:1 Sunderland (Jones dk. 82)
Newcastle (Owen dk. 19, Carrol dk 78) 2:2 West Ham (Bellamy dk 29, Cole dk 55)
Msimamo wa ligi baada ya mechi za jana upo hivi:

No comments: