Sunday, January 11, 2009

Kili Starz kibaruani

Timu yetu ya taifa ya Tanzania Bara leo inashuka uwanjani kumenyana na mahasimu wao wakubwa, Harambee starz ya Kenya. Kili watamkosa beki wao mahiri Kelvin Yondani ambae alipewa kadi nyekundu katika mchezo na Uganda.
Hata hivo Kili, ambayo imekuwa ikitandaza soka la hali ya juu, iko fiti kuikabili Kenya wakiwategemea wachezaji wao mahiri mabeki Salum Swedi na Shadrack Nsajigwa, viungo Godfrey Bonny na chuji na mastriker wao hatari Jerryson Tegete na Mrwanda.
Kocha wa kili, Maximo, ana matumaini makubwa ya kuifunga Kenya na kufuzu kwa Fainali.
Mwanaspoti ntakuletea dondoo za mechi hiyo kupitia mtandao huu leo jioni.
Mechi nyingine ya nusu fainali ni kati ya Uganda na Burundi
Kila la heri Kili Starz

No comments: