Sunday, January 11, 2009

Spain nako, mmh

Huku kwenye Spanish Primera division, Sevilla iliyokuwa ikicheza na watu 10 uwanjani baada ya kiungo Enzo kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 35, ilijikuta ikianza kufungwa goli na Deportivo la Coruna katika dakika ya 34 kabla ya kucharuka na kuichapa Depor goli 3-1. Magoli ya Sevilla yalifungwa na Luis Fabiano, Fredy Kanoute na Renato.
Valencia nayo ikicheza home ground, ililazimishwa sare ya goli3-3 na Villa Real. Magoli ya Valencia yalifungwa na Baraja dk 1, Villa dk 10 na Edu dk 79 huku Villa wakifunga kupitia kwa Fabricio dk 45, joseba dk 76 na kindaa aliekuwa Man U, Giuseppe Rossi dk 84 kwa mkwaju wa penati.
Leo Miamba Barcelona itakuwa ugenini kwa Osasuna huku Real Madrid wakiwa ugenini kwa Mallorca.
Mechi zingine za Spanish Primera itakuwa kama hivi:
Numancia : Getafe
Real Betis : Malaga
Atletico Madrid : Athletic Bilbao
Sporting Gijon : Valladolid
Racing Santander : Recreativo Huelva
Espanyol : Almeria
Kwa msimamo wa Spanish Primera, kongoli hapa chini:

No comments: