Tuesday, January 13, 2009

Kili chupuchupu

Hadi tunakwenda mitamboni dakika ya 30, Kili Stars 1, Burundi 1. Ni half time, kili ishachapwa 2-1 Dakika ya 40, kili wanaongoza 3-2 Mpira umekwisha na Kili stars imeibuka kidedea kwa goli 3-2 na hivo kuondoka na kitita cha dola za kimarekani 10,000 kama zawadi ya mshindi wa 3. HONGERA KILI STARS

Ni Man Yu - Torres

Striker mkali wa wazee wa the Kop; Fernando Torres, Liverpool ana amini kuwa mashetabi wekundu wa Manchesta wanao uwezo mkubwa wa kuchukua ubingwa kwa msimu mwingine.
Torres alisema hayo baada ya Man kuonyesha kiwango cha juu na kuisambaratisha Chelsea kwa goli 3-0!
Man yu wako katika nafasi ya 3 kwenye msimamo wa ligi lakini wana mechi 2 mkononi, dhidi ya Wigan na Bolton, ukilinganisha na vinara Liver. Man wakishinda viporo vyao watakuwa wanaongoza kwa point 1.
Torres anaamini kuwa mechi kati yao na Man Yu Machi 14 ndo itakayoamua bingwa.

Monday, January 12, 2009

Yanga kidume

Timu ya Yanga ya Dar ndio club kilichotoa wachezaji wengi zaidi katika michuano ya CECAFA inayoendelea nchini UG. Yanga ina kikosi kamili na reserve katika timu hizi za taifa ikiwa na jumla ya wachezaji 14! Yanga ina wachezaji katika timu za Kili stars, Zanzibar heroes na Harambee stars. Wachezaji hao ni pamoja na Nsajigwa, Chuji, Bonny, Bakari, Tegete, Makasi, Maftah na Ngassa. Zanzibar Heroes in Abdi Kassim na Haroub Cannavaro wakati Shikokoti, Baraza, Owino na Njoroge wanaiwakilisha Kenya.

Westham watosa dau la Man City

West Ham kwa mara ya pili wametosa dau la paundi milioni 9 za uingereza kwa ajili ya kumuuza staika wao Graic Bellamy kwenda Manchester City. City, yenye kumilikiwa na matajiri waarabu wa Abu Dhabi United Group iko katika mikakati ya kuimarisha kikosi chao ambacho mwenendo wake katika ligi hauvutii. City pia wanamuwania Roque Santa Cruz wa Blackburn Rovers.

Mutajiju, sisi tunakamua

Huu ndo uzalendo

Waarabu wa Oman juzi usiku waliingia mitaani kusherehekea kufuzu kucheza nusu fainali ya kombe la Arabia Gulf Cup. Gari karibu zote nchi nzima, at least zina sticker au bendera ya timu ya taifa toka mashindano hayajaanza. Kama picha invojieleza, watu nao wamejipamba kwa rangi za bendera ya nchi yao. Laiti kama bongo tungekuwa na uzalendo wa hivi......!

Barca chupuchupu

Barcelona jana waliponea chupuchupu kudraw na timu ya mkiani Osasuna baada ya Messi kufunga goli la ushindi dakika ya 85 ya mchezo. Barca walianza kufunga kupitia kwa striker wao Eto'o kabla Osa hawajasawazisha na kuongeza la pili kupitia kwa Flano na Pandiani. Barca walisawazisha goli la pili kupitia kwa Xavi dakika ya 80 kabla M essi hajaipatia ushindi.
Naye Raul jana alifunga goli lake la 500 baada ya kuifungia Real Madrid goli moja huku Arjen Robben na Sergio Ramos wakifunga kuihakikishia Madrid ushindi wa goli 3-0 ugenini dhidi ya Real Mallorca.
Matokeo mengine jana ilikuwa kama hivi:
Msimamo wa Spanisha Primera uko kama hivi:

Becks akipiga Milan ikitoka draw

David Beckam jana alikipiga kwa dakika 89 huku timu yake ya AC Milan ikiambulia draw ya goli 2-2 na AS Roma. Magoli ya AS Roma yalifungwa na Mirko Vucinic katika dakika za 22 na 72 huku mshambuliaji teeneger wa AC Milan, Pato akiifungia Milan magoli yote mawili kwenye dakika za 48 na 53.
Huko Turin, Juventus iliifunga kwa taabu Siena Goli 1-0, goli la Juve likifungwa na Captain wake Allesandro Del Piero.
Matoke kamili ya SEria A ilikuwa kama hivi:
Bologna 1:1 Chievo Verona
Fiorentina 1:2 Lecce
Juventus 1:0 Siena
Napoli 1:0 Catania
Palermo 3:2 Atalanta Regina 2:3 Lazio
Udinese 1:1 Sampdoria As Roma 2:2 AC Milan
Msimamo wa ligi ya Seria A uko kama hivi:

Chelski hoiiiiii

Watoto wa Abramovic jana usiku walikiona cha moto baada ya kuchapwa 3 mtungi na mashetani wekundi wa Manchester.
Nemanja Vidic aliifungia Man U goli la kwanza kwa mpira wa kichwa dakika ya 45 ya kipindi cha kwanza kabla ya Rooney hajafunga la pili baada ya kross maridadi ya Patrice Evra katika dakika ya 63.
Berbatov alihakikisha ushindi unabaki Old Traford baada ya kufunga goli la tatu kutokana na mpira wa adhabu wa Ronaldo.
Chelsea ambao walionekana kupooza walishindwa kabisa kuisumbua ngome ya Man U.
Katika mechi nyingine ya mapema jana jioni, Wigan wakiwa home ground JJB Stadium, waliiliza Tottenham goli moja bila na kuiongezea matatizo mkiani mwa ligi. Goli la Wigan lilipatikana katika dakika za majeruhi kupitia kwa Maynor Figueroa.
Kwa msimamo wa ligi ya Uingereza kong'oli hapa: http://soccernet.espn.go.com/tables?league=eng.1&cc=4716

Sunday, January 11, 2009

Amuiga Kanoute

Mchezaji huyu wa timu ya Taifa ya Oman; Bader Al Maymani, akishangilia bao lake katika michuano inayoendelea ya Arabian Gulf Cup dhidi ya Bahrain kwa staili ya 'Kanoute' ya kuonyesha T-shirt yake yenye maandishi ya kuunga mkono Palestina katika vita vinavyoendelea dhidi ya Israel. T-shirt ya Kanoute inasomeka 'Falestine' na ya Bader inasomeka 'Tuko pamoja na Gaza'. Hata hivo, Bader, tofauti na ilivokuwa kwa Kanoute, hakupigwi faini zaidi ya kusifiwa na ujasiri wake.
Katika mechi hiyo Oman ilishinda 2-0.

Kili Starz nje Cecafa

Mpira umekwisha na Kili stars wamechapwa bao 2-1. Dan Mrwanda ndo kaifungia Kili bao la kufuta aibu. Salum Swedi amepewa kadi nyekundu yenye utatanishi. Hivo Kili wanasubiri atakae fungwa kwenye mechi kati ya wenyeji Uganda na Burundi. Kila la Heri Kili kwenye kuwania hiyo dola 10,000. Kilimanjaro stars iko nyuma kwa bao 2-0 dhidi ya timu ya Harambee stars ya kenya. Kipindi ni cha kwanza.

Becks ndani ya Milan leo

Huko Italia katika ligi ya Seria A, David Beckam, leo anatarajia kuanzia benchi wakati timu yake ya AC Milan itakapokwaana ugenini na AS Roma. Wakati AC wakicheza leo, mahasimu wao wa Milan, Inter Milan, jana wanusurika kula kichapo toka kwa Cagliari baada ya Zlatan Ibrahimovic kusawazisha bao katika dakika ya 77 baada ya Robert kuwafungia Cagliari katika dakika ya 65. Huko Genoa nako, Genoa waliibuka kidedea baada ya kuwaliza Torino bao 3-0. Mechi za leo itakuwa kama hivi: Bologna : Chievo Verona Fiorentina : Lecce Juventus : Siena Napoli : Catania Palermo : Atalanta Reggina : Lazio Udinese : Sampdoria As Roma : AC Milan Kwa msimamo kamili wa ligi ya Seria A, kong'oli hapa chini: http://soccernet.espn.go.com/tables?league=ita.1&season=2008&cc=4716

Spain nako, mmh

Huku kwenye Spanish Primera division, Sevilla iliyokuwa ikicheza na watu 10 uwanjani baada ya kiungo Enzo kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 35, ilijikuta ikianza kufungwa goli na Deportivo la Coruna katika dakika ya 34 kabla ya kucharuka na kuichapa Depor goli 3-1. Magoli ya Sevilla yalifungwa na Luis Fabiano, Fredy Kanoute na Renato.
Valencia nayo ikicheza home ground, ililazimishwa sare ya goli3-3 na Villa Real. Magoli ya Valencia yalifungwa na Baraja dk 1, Villa dk 10 na Edu dk 79 huku Villa wakifunga kupitia kwa Fabricio dk 45, joseba dk 76 na kindaa aliekuwa Man U, Giuseppe Rossi dk 84 kwa mkwaju wa penati.
Leo Miamba Barcelona itakuwa ugenini kwa Osasuna huku Real Madrid wakiwa ugenini kwa Mallorca.
Mechi zingine za Spanish Primera itakuwa kama hivi:
Numancia : Getafe
Real Betis : Malaga
Atletico Madrid : Athletic Bilbao
Sporting Gijon : Valladolid
Racing Santander : Recreativo Huelva
Espanyol : Almeria
Kwa msimamo wa Spanish Primera, kongoli hapa chini:

Premier League mbinde tupu

English premier league inaendelea leo kwa mechi kali kati ya mashetani wekundu, Man United wakiwakaribisha wahasimu wao toka London, vijana wa kitajiri, Chelsea katika uwanja wa Old Traford.
Mechi hiyo inayotarajia kupigwa saa moja kamili kwa saa zetu za Afrika Mashariki inategemewa kuwa kali sana.
Sir Alex anatarajia mechi itakuwa kali sana na katika mahojiano na wahandishi jana, alidai kuwa hatajali kuingia mwenyewe uwanjani kukipiga ili tu timu yake ipate ushindi.
Mdau ntakuwa nawaletea vidokezo muhimu na magoli kadri mechi itakavokuwa inaendelea hapa hapa.
Mdau Ayoub wa Mwanza najua tumbo joto leo maana ni shabiki mkuu wa Man YU!
Katika mechi za jana, Liverpool walivutwa shati na vijana wa mkiani Stoke city kwa kutoka suluhu, Arsenal wakiokolewa na 'super-sub' wao Niclas Bendtner katika dakika za lala salama baada ya kupoke pasi ya Van persie na kuwafunga Bolton 1-0. Newcastle walitoka draw ya 2-2, huku Everton wakiibuka na ushindi wa goli 2-0 dhidi ya Hull na Black Cats sunderland wakisubiri hadi dakika za majeruhi kusawazisha dhidi ya mahasimu wao Middlesbrough.
Matokeo kamili ni kama hivi:
Stock City 0:0 Liverpool
Arsenal (Niclas Bendtner dk. 84)1:0 Bolton
Aston Villa (Davies dk19, Carson dk41 o.g) 2:1 West Brom (Morrison dk. 49)
Everton (Fellaini dk. 47, Cahill dk. 58 2:0 Hull
Middlesbrough (Alves dk. 45 1:1 Sunderland (Jones dk. 82)
Newcastle (Owen dk. 19, Carrol dk 78) 2:2 West Ham (Bellamy dk 29, Cole dk 55)
Msimamo wa ligi baada ya mechi za jana upo hivi:

Kili Starz kibaruani

Timu yetu ya taifa ya Tanzania Bara leo inashuka uwanjani kumenyana na mahasimu wao wakubwa, Harambee starz ya Kenya. Kili watamkosa beki wao mahiri Kelvin Yondani ambae alipewa kadi nyekundu katika mchezo na Uganda.
Hata hivo Kili, ambayo imekuwa ikitandaza soka la hali ya juu, iko fiti kuikabili Kenya wakiwategemea wachezaji wao mahiri mabeki Salum Swedi na Shadrack Nsajigwa, viungo Godfrey Bonny na chuji na mastriker wao hatari Jerryson Tegete na Mrwanda.
Kocha wa kili, Maximo, ana matumaini makubwa ya kuifunga Kenya na kufuzu kwa Fainali.
Mwanaspoti ntakuletea dondoo za mechi hiyo kupitia mtandao huu leo jioni.
Mechi nyingine ya nusu fainali ni kati ya Uganda na Burundi
Kila la heri Kili Starz